Monday, February 11, 2013

SMS ZA MAPENZI NEW


1. Weupe wa penzi lako ni kama mwezi angani.Ucheshi na mahaba yako nifananishe na nini? Kupata mfano wako hatotokea amini. Elewa mimi  ni wako sikuachi asilani.

2. Najiuliza kila leo hivi ni mimi tu kimeo katika dunia hii ya leo maana kila leo nayempata huishia kunipa ahadi kila leo, mpenzi kila siku waniaidi mara nitakupa leo mara kabla ya machweo, hivi ni lini utanipa jibu la uhakika nakunipa mapenzi ya uhakika nipate farijika? Nakupenda mpenzi.

3. Hakika mtoto umeumbika mithili ya malaika japo mbinguni sijafika lakini nauhakika kwa kila mwanaume aliyeumbika na kukamilika akikuona lazima udenda utamtoka, naomba japo yako dakika nipate kukueleza moyoni yaliyonifika kwani siwezi tena kuficha jinsi navyokupenda, nakupenda amini kwako nimefika!

4. Nimezunguka pande zote za Tanzania macho nikiangaza kumsaka mrembo wakumkabidhi yangu nafsi na kulila tunda lake kwa nafasi huku nikimpa mahaba yangu ya dhati na sikuwahi kuhisi kama wewe ndiye ungeiteka yangu nafsi, nakupenda sweetie.

5. Mpenzi nimekumiss jamani, sipati meseji wala simu sijui kwanini, nikikumbuka tunayofanyaga kitandani, natamani ungekuwa nami pembeni nakunipa mahaba yasiyo kifani, nakupenda si utani hani

6. Sijui nikuekleza namna gani uelewe yaliyionijaa moyoni kwani kila nifikiriapo kwanini una walakini na hutaki kuniamini kama wewe pekee ndiye ninayekupa mahaba yangu makini, mpenzi rudisha yako imani ni wewe pekee nayekupenda hapa duniani!

7. Ukweli lazima nikwambiye kwa kuwa sina kimbilio nakupenda kijana mwenzio sijui kwanini hutaki kukisikia changu kilio, namwomba Mungu kila kukicha usikiye changu kilio, nakupenda na kama kukueleza hili nakukosea nisamehe kwani si langu kusudio,luv u mwaah.

8. Naamini uatakuwa umerejea kwenye yako makazi na umechoka na kazi, tafadhali badili yako mavazi , bafuni ingia upate maji kujimwagia, natamani kuja kukusaidia mgongo kuusugua na chakula kukuandalia lakini siku haijawadia, nakupenda dear!

9. Kwa kawaida busu la mafanikio hubusiwa usoni, busu la amani hubusiwa mashavuni, busu la upendo hubusiwa mdomoni, busu la mapenzi hubusiwa shingoni, Je wapi nikubusu ili ulale kwa raha sweet ?

10. Mapenz c pombe lkn yanalewesha,wala c dawa lkn yanaponyesha,wala c maradhi lkn yanaua,wala c kifo lkn yanaliza,wala si katuni lkn yanafurahisha,wala c fimbo lkn yanaumiza.Ni mimi tu mwenye mapenzi ya kweli kwako,Nipende daima mpenzi!!

11. USikimbie nyuki ukakosa asali, utamu wa samaki ni kula na wali,usizidishe siki akawa mkali.
Ni mimi niliye na dhiki nakujulia tu hali.Je,unaendeleaje sakafu wa moyo wangu?

12.Hakika nakwambia mpenzi wanaokutamani ni wengi lakini ni mimi tu mwenye hayo mapenzi ya kweli.ziba masikio na usiwasikilize,nia yao watugombanishe.Nipende daima laaziz wangu!!

No comments:

Post a Comment